Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew amewataka wakazi wa kata za Nyangokolwa na Somanda kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za kishondo Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuchapa kazi na kuboresha huduma za kijamii.
Aidha, Mhandisi Kundo pia amewasisitiza kuchagua viongozi wanaotokana na CCM, ikiwemo yeye pamoja na Wagombea Udiwani ili washirikiane kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea Maendeleo.
Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nyakati tofauti kwenye Mitaa ya Bipyai na Nyaumata, Mhandisi Kundo amesema Mgombea Urais Dk. Samia amedhamiria kuboresha Uchumi na kuimarisha miundombinu ya kijamii ili kurahisisha utoaji wa huduma.
Mhandisi Kundo amesema kuwa endapo wananchi watampigia kura za kishindo Dk. Samia ataboresha huduma za kijamii ikiwemo kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa Umeme, Maji, Barabara na mawasiliano.

"CCM imejikita kutatua changamoto za wananchi, hakuna nongwa, tumefanikiwa kuvuta kutoka Ziwa Victoria, tukimaliza tunavuta Maji kwenye miji yetu na fmilia zisizo na uwezo wa kuvuta Maji, tutawapatia pampu za Maji ili nao wapate huduma ya Maji safi na salama" amesema na kuongeza.
"Dk. Samia ameonyesha dhamira ya kweli na uchungu wa Maendeleo kwa wananchi, anatosha...tumpe kura za kushindo, kura yako iwe sauti yako, tunaenda kupiga kura sababu tuna Wagombea ambao wanatosha na wako tayari Kupamba kwa maslahi ya wananchi."
Mhandisi Kundo amesema akiwa wanauwahamasisha kumpatia kura Dk. Samia ili atuongoze kwa miaka mitano jambo ambalo ni Deni kwake na wananchi ili awatumikie kuleta Maendeleo.
Ameongeza kuwa mwenye haki akitawala, wananchi hupata Maendeleo huku akisisitiza Kuchagua viongozi mwenye sifa za Uongozi wanaotokana na CCM ili washirikiane katika mnyororo wa Maendeleo.
Mwisho.
0 Comments