Header Ads Widget

BILIONI 54 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI KIGOMA UJIJI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI ya manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 53.4 kwa ajiili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoajii huduma katika manispaa hiyo ambapo jumla ya miradi 57 ya kimkakati imetekelezwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji, Kisena Mabuba akitoa taarifa kwa waandishi wa habari alisema kuwa katika miradi hiyo yote imeshaanza kutelezwa na  tayari baadhi ya miradi imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo ofisi za watendaji wa kata na hospitali ya Manispaa ambayo pia imeanza kutoa huduma

Mabuba alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo miradi ya  soko la Mwanga litakalojengwa sambamba na Mwalo wa Katonga itakayogharimu shilingi Bilioni 16 itafungua uchumi wa manispaa hiyo kama lango la mkoa katika  kuchochea shughuli za biashara na uchumi, kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi na  kutekeleza dipromasia ya uchumi kwa nchii za ukanda wa maziwa makuu 

Akizungumza katika ziara hiyo Afisa Elimu shule za msingi wa manispaa hiyo, Richard Mtauka alisema kuwa idara ya elimu ya manispaa hiyo imepokea jumla ya shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya nne  huku shule 10 zikipokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mipango na Uratibu  wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Julius Ndele alisema kuwa katika ziara hiyo ambapo waandishi wa habari walitembelea miradi 14 ni sehemu ya miradi 57 ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 51.7  Kimetolewa na serikali kuu na shilingi Bilioni  2.1 ni kutokana na mapato ya ndani.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI