Header Ads Widget

ENG. KUNDO ASAKA KURA ZA CCM KWA WAJASIRIAMALI MWAKIBUGA.

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi mjini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia) akinunua nyanya toka kwa wajasiriamali katika mtaa wa Mwakibuga, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi mjini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew, akiwa kwenye mwendelezo wa kampeni, amepita katika soko la wafanyabiashara ndogondogo wa mbogamboga, miwa na matunda na kuwaomba kura ili wachague viongozi wanaotokana na CCM. 


Mhandisi Kundo amewataka wafanyabiashara hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kumchagua Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge (Mhandisi Kundo) pamoja na Diwani wa CCM (David Masanja) ili wawawekee Mazingira mazuri ya kufanyia biashara.


"Jitokezeni kwa wingi Oktoba 29, 2025 ili mkachague viongozi waotokana na CCM waweze kuwaletea Maendeleo... Na katika mtaa wa Mwakibuga tutaweka taa za Barabarani ili mfanye Biashara mpaka usiku" amesema Mhandisi Kundo. 


Amesema kuwa agenda ya CCM ni kutatua changamoto za wananchi na kwamba wameandaa Ilani ya kuchochea Mapinduzi ya kisasa kupitia sayansi na teknolojia, kuimarisha mawasiliano na sekta ya Afya ili wananchi wasipate changamoto. 


Pamoja na kuwaomba kura WAJASIRIAMALI hao, Mhandisi Kundo pia aliwachangia kwa kutoa fedha ili kununua bidhaa zao ikiwemo nyanya, kabeji, miwa na bamia.

Mwisho. 


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi mjini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Kundo Mathew akinunua na kula miwa pamoja na Wananchi wa Mtaa wa Mwakibuga wakati akisaka kura za CCM.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI