Header Ads Widget

KUSUSIA UCHAHUZI HASARA KUBWA NIOMBE WANACHADEMA JITOKEZENI OKTOBA 29 KUPIGA KURA NICHAGUENI MIMI UBUNGE IRINGA MJINI -CHIKU ABWAO

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha ACT- wazalendo Chiku Abwao amesema kuwa kususia uchaguzi ni kukosa mahala pa kusemea changamoto za wananchi ambao wanataka kuwatumikia.

Abwao alisema hayo wakati akifanya kampeni katika eneo la stendi ya zamani mjini Iringa na kueleza kuwa chama cha ACT wazalendo kilisema hakiwezi kususia uchaguzi kwa sababu kususia uchaguzi ni sawa na mkulima kulima shamba na kuachia ngedere.

Alisema kuwa wameamua kushiriki uchaguzi huku wakipambana kulinda kura zao lengo likiwa ni kwenda bungeni kutetea haki za wananchi.

"Kususia uchaguzi hakuna faida na hatuwezi kufanikiwa kwa kususa, tulisusia bunge la katiba lakini CCM waliamua kutengeneza katiba yenye ubinafsi yenye mlengo wa chama kimoja ambayo pia wameshindwa kuitumia na kurudi katika matumizi ya katiba ya zamani"alisema 

"Nawaomba siku ya tarehe 29, oktoba mjitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na mnichague mimi ili nikawasemee ndani ya bunge na tuweze kuzitatua changamoto zinazokabiri wananchi, niwasisitize  muweke nguvu katika kuchagua viongozi wa upinzani ambao wako tayari kuwatetea wananchi"alisema

"Mimi nimekuwa mpambanaji tangu waka 1992 napambania mfumo wa vyama vingi ili tuweze kupata utetezi katika bunge la jamuhuri la tanzania".

Aidha aliongeza kuwa katika kupambania ushindi 2025 lengo la ACT ni kutaka kuirudisha Tanzania katika uhalisia wa mwananchi kwanza,kwa kupata maslahi sawa bila kuweka vikwazo 

Abwao alisema kuwa mfumo wa vyama vingi upo kwa ajili ya kutetea wananchi na kuikosoa serikali ili pale inapokosea iweze kujirekebisha, hivyo ni harasa kubaki na chama kimoja cha wawakilishi ndani ya bunge 

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI