Header Ads Widget

KATAMBI AKUTANA NA BALOZI WA BURUNDI NCHINI TANZANIA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Burundi nchini Tanzania,Mhe. Balozi Leontine Nzeyimana, ambapo wamezungumza masuala mbalimbali ikiwemo uwepo wa kambi za Wakimbizi hapa nchini,Udhibiti na utoaji elimu ili kuzuia uhalifu na Ustawi wa Jamii ya Wakimbizi wa Burundi waliopo hapa nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa wizara hiyo,Ayoub Mohammed Mahmoud,Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Maduhu Kazi na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje,Evans Magoiga.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo,Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mtumba jijini Dodoma.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI