Polisi walisema siku ya Jumatatu asubuhi, mzee wa miaka 56, akiwa na upinde na mishale, alikaribia maafisa kwenye lango la Ikulu na kuamriwa kujisalimisha. Badala yake, alisonga mbele na kumdunga mshale afisa Ramadhan Matanka kwenye mbavu.
Polisi huyo alipelekwa hospitali mara moja lakini alifariki alipokuwa akipata matibabi, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
Shambulio hilo limeibua maswali kuhusu uwezekano wa kudorora kwa usalama kwani Ikulu ni mojawapo ya maeneo yenye ulinzi mkali zaidi nchini Kenya.
Mwili wa PC Matanka sasa uko katika chumba cha kuhifadhia maiti na uchunguzi wa maiti utafanywa baadaye.
Uchunguzi pia unaendelea kubaini chanzo cha shambulio hilo.
Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kwamba polisi aliyekufa alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakichunguza magari yaliyokuwa yakiingia Ikulu.
0 Comments