Header Ads Widget

ZITTO ACHARUKA KUKWAMA UJENZI KIWANDA CHA MELI KIGOMA.

Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia) akimnadi Mgombea udiwani wa kata ya Bangwe kwa tiketi ya chama hicho, Abdallah Rajab Mandanda katika mkutano uliofanyika viwanja vya Camara Bangwe manispaa ya Kigoma mjini.




Na Fadhili Abdallah,Kigoma


MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kigoma kwa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka kuharakishwa kwa mradi wa ujenzi wa cherezo (Kiwanda) cha kutengeneza meli katika eneo la Katabe Manispaa ya Kigoma Ujiji kwani mradi huo ambao una faida kubwa kwa uchumi wa wananchi wa mkoa Kigoma umechelewa kwa muda mrefu.


Zitto alisema hayo akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kamara Bangwe manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kutainua uchumi na mzunguko wa fedha kwa wananchi wa jimbo hilo na maeneo mengine ya mkoa Kigoma.


Mgombea huyo alisema kuwa pamoja na faida zilizopo katika mradi huo lakini mradi umekuwa ukisuasua kutekelezwa na kukatisha tamaa wananchi hivyo ameitaka serikali kuyaishi maneno yake kwani mradi umekuwa ukisemwa sana kulingana na faida zake lakini utekelezaji wake bado changamoto kubwa.


“Mradi huu una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 600 pamoja na chelezo pia meli mbili kubwa zitakazojengwa, Mradi huu ni fursa kubwa kwa mji wetu kwani shipyards ni vichocheo vya maendeleo ya miji. Ujenzi wa meli ukianza karibu watu 1,000 watakuwa wanafanya kazi kila siku, hata hivyo maneno ni mengi kuliko vitendo tunataka kuona utekelezaji unafanyika haraka,”Alisema Zitto Kabwe.


Pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati mgombea huyo amekemea tabia ya serikali kuchukua maeneo ya watu ambayo uwekezaji unafanyika bila kulipa fidia na kwamba jambo hilo linakwenda kinyume na katiba ya nchi hivyo ametaka maeneo yanayochukuliwa lazima yalipwe fidia wakati huu ardhi inapanda thamani na watu wanaona ardhi hizo kama mitaji yao.


Zitto alisema kuwa Ili kukabiliana na ucheleweshaji huo anahitajika mbunge ambaye atasimama ni kuipigia kelele serikali kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa wakati hivyo amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema kuwa mkoa Kigoma unahitaji wabunge wanaoweza kupambani na kujenga hoja miradi kuletwa Kigoma lakini kusimamia kwa karibu kuhakikisha miradi inatekelezwa.


Nondo alisema kuwa kwa sasa miradi mikubwa inatekelezwa Kigoma ukiwemo mradi wa reli ya kisasa (SGR) hivyo ni lazima mkoa upate wabunge watakaoweza kusimamia fedha hizo zifanye kazi bila kuchepushwa au kuwepo kwa matumizi mabaya hivyo akataka Zitto Kabwe achaguliwe akasimamie hilo.


Mwisho.


Mwenyekiti wa ngome ya vijana chama cha ACT Wazalendo Abdul Nondo akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombe ubunge wa chama hicho jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI