Header Ads Widget

NJALU ANADI ILANI YA CCM NA KUWATAKA ITILIMA KUSHIKAMANA BAADA YA UCHAGUZI.

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga akinadi sera za CCM kwenye Mkutano ya kampeni.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba baada ya Uchaguzi washikamane kuijenga wilaya ya Itilima.


Aidha, amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anasimamia Ilani ya CCM pamoja kusimamia miradi ya Maendeleo ambayo itatakelezwa kwa manufaa ya wananchi.


Njalu ameyasema hayo kwa nyakati tofauti jana wakati akinadi sera za CCM kwa Wakazi wa kata ya Mbita, Nhobola na Lugulu na kuwasisitiza kumpigia kura za kishindo Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan.



"Pamoja na Ilani nzuri tuliyoinadi katika kata zote za jimbo la Itilima, ninawaomba sana ndugu zangu tupendane, tushirikiane na tushikamane kuijenga Itilima yetu tusikubali mtu yoyote kutuvuruga sisi agenda yetu ni maendeleo..." amesema Njalu na kuongeza.


"kwa Umoja na Upendo huu tulionao tujitokeze kwa wingi tarehe 29, Oktoba tukampe kura nyingi Dk. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais,Tupige kura ya ndiyo kwa Mbunge wenu (Njalu) na tuwape kura za kutosha madiwani wa CCM"


Mwisho.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI