Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WA MISAADA WATUMIA PUNDA KUWAFIKIA WAATHIRIWA WA MAPOROMOKO YA ARDHI SUDAN

 

Wafanyakazi wa misaada kwa kutumia usafiri wa punda wamefanikiwa kuwasilisha msaada wa kwanza wa kibinadamu kwa manusura wa maporomoko ya ardhi yaliyoripotiwa kuua mamia ya watu katika kijiji cha milimani huko Darfur magharibi mwa Sudan.

Mvua kubwa na mafuriko yaliyokumba kijiji cha Tarasin yalisababisha maafa siku ya Jumapili huku punda wakitumia kama njia pekee ya kufikia familia zilizoathiriwa.

"Familia huko Tarsin zimepoteza kila kitu. Iliwachukua wahudumu wetu zaidi ya siku kupitia njia yenye mawe, matope na milima kufikia wakaazi hawa walioathiriwa," alisema Francesco Lanino, kutoka shirika la misaada la Save the Children.

Bado haijabainika ni watu wangapi walikufa.

Kundi lililojihami linalodhibiti eneo hilo linakadiria kuwa watu 1,000fariki katika maporomoko hayo, lakini wizara ya afya inasema ni miili miwili pekee ndio imepatikana.

Siku ya Alhamisi, viongozi wa raia wa eneo hilo walisema kuwa wameopoa na kuzika miili ya mamia ya watu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI