Header Ads Widget

RUBIO ASEMA MAREKANI ITAYALIPUA MAKUNDI YA WAHALIFU WA KIGENI

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema nchini hiyo "italipua" makundi ya uhalifu ya kigeni ikihitajika, ikiwezekana kwa ushirikiano na mataifa mengine.

"Sasa watatusaidia kuwasaka watu hawa na kuwalipua, ikiwa ni hivyo," Rubio alisema wakati wa ziara ya Ecuador.

Pia alitangaza kuwa Marekani itayaorodhesha magenge mawili makubwa ya wahalifu nchini Ecuador, Los Lobos na Los Choneros, kama mashirika ya kigeni ya kigaidi.

Kauli jiyo inakuja siku chache baada ya vikosi vya Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya boti moja katika bahari ya Caribbean.

Ikulu ya White House inasema iliwaua walanguzi 11 wa dawa za kulevya, lakini haikutoa utambulisho wao.

Usiku wa Alhamisi, idara ya ulinzi ilishutumu ndege mbili za kijeshi za Venezuela kwa kuruka karibu na meli ya Marekani katika "hatua ya uchochezi iliyopangwa kuingilia shughuli zetu za kukabiliana na ugaidi".

Venezuela bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

Marco Rubio alipoulizwa ikiwa wasafirishaji haramu kutoka nchi ambazo ni za washirika wa Marekani, kama vile Mexico na Ecuador, wanaweza kukabiliwa na majeshi ya Marekani.

Alisema "serikali rafiki" zitatusaidia kuwatambua wasafirishaji haramu. "Rais amesema anataka kupambana na makundi haya kwa sababu yamekuwa yakitushambulia kwa miaka 30 na hakuna aliyechukua hatua. "Lakini hakuna haja ya kufanya hivyo katika hali ambapo wahusika wanatoka katika nchi amayo ni mshirika wetu, kwa sababu serikali rafiki zitatusaidia."

Serikali za Ecuador na Mexico hazijasema zitasaidia katika mashambulizi ya kijeshi.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI