Header Ads Widget

PAPA LEO XIV NA RAISI WA ISRAEL WAJADILI 'HALI MBAYA YA GAZA'

 

Papa Leo XIV na wanadiplomasia wake wakuu wamezungumza na rais wa Israeli siku ya Alhamisi na kumfahamisha kwamba suluhisho la serikali mbili ndio "njia pekee ya kumaliza vita" vya Gaza huku Vatican ikitaka usitishaji wa kudumu wa mapigano hayo, kuachiliwa kwa mateka wote na kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina waliokumbwa na njaa.

Vatican ilitoa taarifa ya kina isivyo kawaida kufuatia mkutano wa Leo na Rais wa Israeli Isaac Herzog, ambaye pia alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Herzog, kwa upande wake, alisema alimwomba Leo kukutana na familia za mateka, na akatoa wito wa kuimarishwa juhudi za kimataifa ili kuwaachilia huru.

Papa Leo XIV alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo mwezi Julai baada ya shambulizi la kigaidi la Israel kulivamia kanisa pekee la Kikatoliki huko Gaza na kuua watu watatu na kumjeruhi kasisi wa parokia hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI