Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS DKT NCHIMBI AFANYA MAZUNGUZO NA BALOZI WA CUBA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne Vera, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 12 Machi 2026.
 
Mazungumzo hayo, yamelenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Cuba, ambao unatimiza miaka 64.  Cuba na Tanzania zimekuwa zikishirikiana katika Sekta mbalimbali za kimkakati kama vile Elimu, Afya, Utalii pamoja na Kilimo.
 
Tanzania na Cuba kwa miaka mingi zimeendelea kuwa na mahusiano na maelewano ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia katika ngazi ya nchi mbili, kikanda na kimataifa. Tanzania na Cuba zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1962 mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru mwaka 1961.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI