Header Ads Widget

TUNDU LISSU KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

 

Mwenyekiti wa upinzini nchini Tanzania Tundu Lissu, anapandishwa kizimbani, Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing - PH).

Kesi ya kiongozi huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imepangwa kusikilizwa leo, Jumatatu Agosti 8, 2025 katika hatua hiyo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru.

Lissu, alikamatwa mwezi Aprili na kushtakiwa kwa uhaini, shitaka ambalo akikutwa na hatia hukumu yake ni kifo, kutokana na kudaiwa kutoa wito kwa wafuasi wake kuzuia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Lissu, ambaye alipigwa risasi 16 katika shambulio la mwaka Septemba 2017 katika eneo la makazi ya viongozi mjini Dodoma na kesi yake imekuwa ikifuatiliwa na mataifa ya kigeni zikiwemo nchi za Ulaya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI