Header Ads Widget

SIRRO ATUMA SALAM TIMU ZA LIGI KUU

 

Kikosi cha timu ya Mashujaa kilichotambulishwa katika Tamasha la timu hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro ametuma salam kwa timu za ligi ya Tanzania bara kuwa wasiichukulie poa timu ya Mashujaa kutoka mkoani Kigoma kwamba imejiandaa kuhakikisha inafanya vizuri katika ligi ya msimu huu.

Akizungumza katika tamasha la kutambulisha wachezaji wa timu hiyo maarufu kama Mashujaa Day Mkuu huyo wa mkoa Kigoma ametangaza dhamira ya ofisi yake kuiunga mkono timu hiyo sambamba na wananchi wote wa mkoa huo kuungana kwa hali na mali kuhakikisha malengo ya simu hiyo ya kufanya vizuri msimu huu kuelekea ubingwa yanafikiwa.

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akizungumza katika tamasha la Siku ya Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini

“Nimeona wachezaji waliosajiliwa na timu kwa msimu huu ni wachezaji wazuri na wakubwa wakiwemo ambao wamechezea vilabu vyetu vikubwa vya simba, Yanga, Azam, Fountain Gate na wapo wachezaji wamecheza nje ya nchi ikiwemo ligi ya Afrika Kusini hivyo ni wazi timu itatoa ushindani mkubwa msimu huu,” Alisema Mkuu huyo wa mkoa Kigoma.


Katika Tamasha hilo  Timu hiyo ya Mashujaa ilicheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa  na timu ya daraja la kwanza ya Vital’O ya nchi Burundi kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma ambapo Mashujaa waliibuka kwa ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0.

Mabao hayo ya Mashujaa yalifungwa na mshambuliaji wao Ismail Mgunda ambaye msimu huu amerejea kwenye timu hiyo baada ya kusajiliwa na timu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo  katika dirisha dogo msimu uliomalizika .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI