Header Ads Widget

TUME YA UCHAGUZI TANZANIA YAMUONDOA MPINA KATIKA MAJINA YA WAGOMBEA WA URAISI

 

Mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Luhaga Joelson Mpina amekutana na kizingiti kingine baada ya Tume ya Uchaguzi kuondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha urais.

Uamuzi huo wa Tume umetokana na pingamizi lililowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Said Johari dhidi ya Mpina.

Mpina ameondolewa kwenye orodha ya wagombea siku nne tu baada ya kushinda kesi katika Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dodoma alipokuwa akipinga uamuzi wa awali wa Tume wa kumzuia kurudisha fomu ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais.

Kwa mujibu wa taarifa ya ACT Wazalendo, pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilidai kwamba Mpina hakuwa na sifa ya kuwa Mgombea wa Urais kufuatia uamuzi wa awali Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Katika taarifa yake kwa umma, ACT Wazalendo kilikitupia lawama Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya mgombea wake Mpina kikidai kwamba mapingamizi hayo hayakuwa na ukweli wala msingi wowote.

Haijafahamika bado ikiwa ACT Wazalendo watarudi mahakamani kupinga tena pingamizi hili jipya la Tume ya Uchaguzi


                         

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI