Header Ads Widget

SIRRO AINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI MWEKEZAJI NA WANANCHI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SERIKALI mkoani Kigoma imeanza kuchukua hatua kuhusu mgogoro wa eneo la Hekta 10,000 ambalo wananchi wa kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wanadaiwa kuvamia eneo la mwekezaji kampuni ya FAZENDA ambayo imekusudia kuwekeza katika mradi wa kilimo kutakiwa kuondoka ili mwekezaji aanze shughuli zake.

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Siro akizungumza na wananchi wa eneo hilo alisema kuwa baada ya kusikiliza pande zote mbili za wananchi na upande wa serikali amechukua uamuzi wa kuwataka wananchi hao kuendele na shughuli zao wakati akiwataka watendaji wa serikali ya wilaya na idara ya ardhi mkoa kumletea taarifa ya nani aliyeanza kuwepo katika eneo hilo.

Wanachi wa kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza wanaodaiwa kuvamia eneo la Mwekezaji wakiwa katika mkutano na Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro

Mkuu huyo alisema kuwa anataka taarifa inayoonyesha hilo lini mwekezaji alipewa eneo hilo  na lini  wananchi walianza kulitumia eneo hilo na kwamba baada ya kupatikana taarifa hizo ofisi yake itatoa maelekezo ya hatua za mwisho za kuchukukua kukabiliana na mgogoro huo.

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambao wanadaiwa kuvamia eneo la mwekezaji na kuanzisha shughuli za uchumi

Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa kuhusu mgogoro huo Mkuu wa wilaya Uvinza, Dinnah Mathamani alisema kuwa Zaidi ya wananchi 800 wamevamia eneo la Hekta 10,529 lililotolewa kwa mwekezaji kampuni ya FAZENDA kupitia Mamlaka ya  uwekezaji na maeneo maalum ya kiuchumi (TISEZA) na kuanza kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na mifugo.

Mkuu wa wikaya Uvinza Dinnah Mathamani akizungumza katika mkutano huo wa mkuu wa mkoa

Mkuu huyo wa wilaya Uvinza alisema kuwa baada ya kuona hivyo   mwaka jana walitoa tangazo kwa wananchi hao kuvuna mazao yao na kuondoka eneo hilo kufikia mwisho mwa mwezi wa Nane mwaka huu ambapo tarehe 20 Agosti Mkuu huyo wa wilaya akifika eneo hilo na kutoa tangazo la wiki mbili wananchi hao kuondoka eneo hilo.

Kufuatia tangazo hilo wananchi hao waliandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu wakilalamikia kuondolewa kwenye eneo hilo bila kulipwa fidia na kuonekana kuwa ni wavamizi wakati hakukuwa na maelekezo yeyote kwa miaka Zaidi ya 15 ambayo wameishi na kuwekeza eneo hilo.


 

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI