Header Ads Widget

MBWAMAJI YAFANYA MABADILIKO KAMATI YA MIUNDOMBINU, YATOA ONYO KWA WANAOJENGA MAENEO YA UMMA

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku' akizungumza katika mkutano huo


Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku' ametoa onyo kali kwa Wananchi wanaovamia maeneo yaliyotengwa rasmi kwa matumizi ya Umma na hifadhi za barabara kuacha mara moja kwani watachukuliwa sheria kali.

Mhe Mwenyekiti huyo amesema hayo katika mkutano wa wazi wa Wananchi wa Mtaa huo wa Mbwamaji mwishoni mwa wiki ambapo pia amefanya mabadiliko ya Kamati mbili ya ikiwemo Kamati ya Ardhi na Kamati ya Miundombinu.

"Katika kuimalisha Kamati hizi nyeti katika Mtaa wetu, Ndugu Vincente Mbalamwezi atakuwa mshauri kwenye Kamati ya Ardhi.

Mbalamwezi mwanzo alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu na nafasi hii ya Uenyekiti wa kamati ya Miundombinu atahudumu ndugu Frances Mwakitalu.

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mbwamaji wakisikiliza na kutoa maoni katika mkutano huo 


Nimefanya hivi sihitaji migogoro ya Ardhi kwenye Mtaa ninao uongoza" Amesema Mhe. Maziku.

Na kuongeza kuwa:

"Upande wa miundombinu sitaki kuona watu wana jenga kwenye barabara na maeneo yaliyotengwa rasmi kwa matumizi ya umma.

Lakini pia, ni lazima tutafute wadau wa kutusaidia upande wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara zetu na mitaro hususani unao toka kwenye makazi ya watu kuelekea baharini, milango ipo wazi tunakaribisha wadau kusaidia katika hilo" amesema Mhe.Maziku.

Aidha, Mwenyekiti Mhe Maziku amesema kwenye maendeleo wote tunakuwa pamoja kwa maendeleo ya mtaa wetu huku pia akiwapongeza viongozi wa dini na wazee wa ndani ya mtaa huo kwa ushirikiano mkubwa tokea alipochaguliwa kuongoza Mtaa huo kwa mara nyingine tena tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku' akizungumza katika mkutano huo








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI