Header Ads Widget

SHULE ZA MANISPAA YA KIBAHA ZATAKIWA KUTOA ELIMU FANISI.

 


Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima App Kibaha.

TAASISI za elimu kwenye Manispaa ya Kibaha zimetakiwa kutoa elimu fanisi kwa wanafunzi ili elimu hiyo iendane na ushindani wa kielimu ulimwenguni.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Mkurugenzi wa Mabispaa ya Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa wakati wa Mahafali ya darasa la saba ya Shule za Msingi Kibaha Independent School (KIPS) Main, Annex na Msangani.

Shemwelekwa amesema kuwa elimu fanisi ni nzuri kwani inamfanya mwanafunzi anapata ujuzi wa kila sehemu hivyo kuweza kuendana na hali ya sasa ya kiteknolojia.

"Tumeona pale wanafunzi wanajifunza darasani, wanajifunza teknolojia na wanajifunza ujuzi mbalimbali hali inayomfanya muhitimu kumudu mazingira yote,"amesema Shemwelekwa.

Kwa upande wake kaimu ofisa elimu Msingi kutoka Manispaa ya Kibaha Adinani Livamba amesema kuwa kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 6,537 wakiwemo 1,132 kutoka shule binafsi wamehitimu elimu ya Msingi.

Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya Njuweni Alhaj Yusufu Mfinanga amesema kuwa kupitia shule hizo za KIPS watatoa ufadhili kwa wanafunzi 12 watakaopata ufaulu wa daraja A kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwenye Shule za Sekondari ya Vuchama Ugweno Islamic iliyopo Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Awali mwalimu Mkuu wa Shule ya KIPS Annex yalipofanyika mahafali hayo Ramadhan Kitambi amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano shule hizo zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kwenye Manispaa, Mkoa na Kitaifa kwa kupata daraja A bora zaidi6 na kuwataka wazazi na walezi kushirikiana na uongozi wa shule hizo ili kuendelea kupata matokeo mazuri ambapo jumla ya wahitimu 160 walitunukiwa vyeti vya kumaliza elimu ya msingi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI