Header Ads Widget

SAMIA ATAJWA UBORESHAJI MIUNDO MBINU YA SHULE KIGOMA.

 

Wanafunzi wa shule ya msingi ukombozi halmashauri ya wikaya Kigoma wakiwa katika uzinduzi wa madarasa manne ya shule hiyo uliofanywa na mwenge wa uhuru.


Na Fadhili Abdallah, Kigoma


IMEELEZWA kuwa uboreshaji wa miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari nchini ni moja ya ajenda kubwa za Rais Samia Suluhu Hassan tangu siku ya kwanza anaingia madarakani ili kurudisha hadhi na heshima ya shule za serikali ambazo zilikuwa zinakimbiwa na wananchi na kuwa na miundo mbinu duni


Kiongozi wa Mwenge wa uhuru mwaka 2025, Ismail Alli Ussi alisema hayo wakati Mwenge wa uhuru ukizindua madarasa manne na matundu sita ya vyoo katika shule ya Msingi Ukombozi halmashauri ya wilaya Kigoma ambapo alisema kuwa kutokana na hivyo serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknlojia imelifanyia jambo hilo kuwa la kipaumbele.


 


Ussi alisema kuwa Rais Samia alidhamiria kuondoa utofauti uliopo baina ya shule za serikali na shule binafsi za kulipia na kwamba hali hiyo imefanikiwa na sasa sehemu kubwa ya shule za msingi na sekondari za serikali zina miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia ambayo inawapa hamasa wananchi kupeleka watoto wao kwenye shule hizo.


Mmoja wa walimu wa shule ya Msingi ukombozi, Anarei  Mosha akizungumza na waandishi wa habari amekiri kuwa uboreshaji wa miundo mbinu katika shule hiyo umechochea wanafunzi kuhudhuria masomo sambamba na wazazi kusimamia watoto wao kuhakikisha wanafika shule.


Mwalim Mosha alisema kuwa kufuatia uboreshaji huo uliofanyika imewapa nafuu sana katika kufundisha kwani idadi kubwa ya wanafunzi wanahudhuria masomo na imesaidia kuinua taaluma katika shule hiyo.


Awali Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Thecla Pascal alisema kuwa kiasi cha shilingi 168.2 milioni zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kupitia mradi wa kuboresha mazingira ya kujifundishia na kujifunzia chini ya wizara ya Elimu (BOOST) na kutekelezwa kwa mradi huo kulilenga kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani katika shule hiyo.


Mwisho.


Kiongozi wa mwenge wa uhuru Ismail Alli Ussi akizungumza katika uzinduzi wa madarasa manne ya shule ya msingi Ukombozi halmashauri ya wilaya Kigoma yaliyotekelezwa kupitia mradi wa BOOST.


Madarasa na vyoo vya shule katika shule ya Msingi Ukombozi halmashauri ya wilaya Kigoma ambavyo vimezinduliwa na mwenge wa uhuru. 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI