Header Ads Widget

DAKTARI WA UPASUAJI AFUNGWA JELA BAADA YA KUKATWA MIGUU YAKE MWENYEW

 

Daktari wa upasuaji wa mishipa ambaye alikatwa miguu amefungwa jela miaka miwili na miezi minane kwa ulaghai wa bima na kumiliki ponografia.

Neil Hopper, 49, alifanya mamia ya upasuaji wa kukatwa viungo kabla ya kukatwa miguu yake mwenyewe mnamo mwaka 2019.

Mahakama iliambiwa kwamba alidanganya kampuni ya bima kwa kudai kuwa na majeraha kwenye miguu yake yaliotokana na ‘sepsis’ (hali inayosababishwa na maambukizi mabaya) wala sio kujiumiza mwenyewe.

Mnamo mwezi Mei 2019 Hopper alikatwa miguu chini ya goti baada ya "ugonjwa wa kushangaza". Ukweli ni kwamba alitumia barafu na barafu kavu kugandisha miguu yake mwenyewe hivyo basi, ikabidi ikatwe, alisema mwendesha mashtaka Nicholas Lee.

Mahakama iliambiwa kuwa Hopper, ambaye alikiri makosa mawili ya ulaghai na matatu ya kumiliki ponografia, alikatwa miguu ili kutekeleza "nia ya kingono".

Jaji James Adkin alisema akitoa hukumu kwamba alikubali kuwa Hopper, ambaye hakuwahi kuwa na kesi za mahakamani hapo awali, alikuwa akijuta maamuzi yake.

Hata hivyo, "kiwango cha madhara" katika video tatu za kukatwa viungo vya mwili chini ya mashtaka ya ponografia, kilikuwa "juu sana", alisema.

Hopper alikatwa miguu yote miwili baada ya kulalamika kuwa miguu yake ilikuwa na maumivu.

Alitibiwa kwa tuhuma za ugonjwa wa ‘sepsis’ kabla ya kuambiwa na madaktari wa upasuaji kwamba alipaswa kukatwa miguu na kufanyiwa upasuaji huo.

Hakuwaeleza madaktari sababu halisi ya majeraha yake, mahakama iliarifiwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI