Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amezungumzia shutuma kwamba Israel "inalenga raia makusudi". "Kinyume chake ni kweli," anasema, akisema kuwa Israel imeangusha "mamilioni ya vipeperushi na kutuma mamilioni ya maandishi" ili kuwafanya raia kuhama mji wa Gaza.
Wakati huo huo, "Hamas inajipandikiza kwenye misikiti, shule, hospitali, majengo ya ghorofa" anasema, ili kuwalazimisha raia "kukaa katika hatari" , "mara nyingi wakiwatishia kwa mtutu wa bunduki".
Akiendelea na madai ya mauaji ya halaiki, Netanyahu anauliza ikiwa nchi inayofanya mauaji ya halaiki inawasihi watu kutoka katika hatari, "Je, Wanazi waliwataka Wayahudi kuondoka?"
Kisha anakana shutuma kwamba Israel inawaua watu kwa njaa huko Gaza kwa makusudi. Iwapo kuna watu wa Gaza ambao hawana chakula cha kutosha ni kwa sababu Hamas "huiba, huihifadhi na kuiuza".
Mapema mwezi huu, tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ilisema Israel imefanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Wizara ya mambo ya nje ya Israel ilishutumu ripoti hiyo kama "iliyopotoshwa na ya uwongo".
Netanyahu amezungumza katika Mkutano Mkuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa.
0 Comments