Takribani watu 260 wanaoshukiwa kuwa matapeli wa mtandaoni wamekamatwa katika operesheni kali iliyotekelezwa katika nchi 14 za Afrika.
Operesheni hiyo, iliyoratibiwa na Interpol na kufadhiliwa na Uingereza, ililenga mitandao ya wahalifu inayotumia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali kuchota pesa kutoka kwa waathiriwa katika ulaghai wa mapenzi, na katika kile kinachoitwa "ulaghai", ambapo waathiriwa wanadanganywa kwa kutumia picha chafu.
"Haichukui muda mrefu kabla ya kujenga uhusiano na mtu fulani... na kwa haraka sana uaminifu huu unasambaratika," mkurugenzi wa uhalifu wa mtandaoni wa Interpol Neal Jetton aliambia kipindi cha Newsday cha BBC, akielezea mbinu za wahalifu hao.
Zaidi ya waathiriwa 1,400 kote nchini Ghana, Kenya, Angola na kwingineko walitambuliwa.
Interpol inakadiria kuwa waathiriwa walipoteza jumla ya karibu $2.8m (£2.1m).
Watu wa rika mbalimbali walichukizwa na walaghai, Jetton aliongeza, lakini "kawaida ulaghai huu huathiri watu wazee".
Wakati wa msako mkali ambao ulifanyika kati ya Julai na Agosti, polisi walitambua anuani za IP, miundombinu ya kidijitali na wasifu wa mitandao ya kijamii unaohusishwa na wanachama wa mashirika ya ulaghai.
Mtandao wa polisi wa kimataifa ulisema umejitolea "kuvuruga na kusambaratisha vikundi vinavyowawinda watu walio hatarini mtandaoni".
0 Comments