Uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya unawatafuta ndugu wa Bi.Angela Julius Mgimwa ambaye amefariki toka tarehe 10/09 /2025 na mwili wake bado umehifadhiwa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa ndugu zake.
Angela alikua amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu na kabla umauti haujamfika alisema nyumbani kwao ni njiapanda ya Tosamaganga, Iringa. Baba yake anaitwa Julius Mgimwa na mama yake anaitwa Cecilia Kalinga (mama alishafariki). Kaka yake anaitwa Sadiki Julius Mgimwa anaishi Iringa.
Angela ana mtoto mmoja wa kiume anaitwa Alvin alizaa na mtu wa Igowole huko Mafinga, mkoani Iringa.
Mpaka umauti unamkuta Agnes alikuwa anaishi kijiji cha Itumbi, wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya.
Kwa yeyote anayefahamu ndugu au jamaa zake tafadhali apige simu nambari 0685859194. Tafadhali sambaza link hii maeneo mbalimbali ili kusaidia ndugu zake wapatikane.






0 Comments