NA AMINA SAIDI,TANGA,
Katika juhudi za kuimarisha umoja ndani ya Chama,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Tanga Ustadhi Rajab Abdul Rahman,ametoa wito kwa wanachama na wagombea walioteuliwa kwenye kura za maoni kuachana na makundi yaliyojitokeza wakati wa mchakato huo,alisisitiza kuwa umoja ni nguzo kuu ya mafanikio pamoja na ushirikiano utawawezesha kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu.
Kutokana na umuhimu wa kushinda uchaguzi,kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa pamoja na kamati za kampeni ngazi ya Kata,Wilaya na Mkoa,Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa wanachama wanapaswa kuacha tofauti zao na badala yake waungane ili kuhakikisha chama kinaoata ushindi wa kishindo.
Kwa upande wake mzee Musa Shekimweri ambaye alikuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa aliwataka wajumbe kuweza kutambua kuwa nafasi ya uchaguzi ni moja tu mtu anapoachwa kwenye kura au kutokuteuliwa ni kwaida wala sio jambo la kutengeneza chuki na kipindi cha kura za maoni makundi pia kawaida ila baada ya hapo wanapaswa kukaa pamoja na kujenga nyumba moja.
Alisema cha kufahamu ni kwamba wagombea wanaweza kujitokeza wengi kwenye kiti Kimoja lakini baada ya hapo atakayekaa kwenye kiti ni mtu mmoja ambaye ndio atakayebahatika tu hivyo hakuna haja ya kugawanyika ndani ya Chama Cha mapinduzi.
Hata hivyo alitoa ombi kwa viongozi wa CCM kuwa wakati wa Uchaguzi tarehe 29 mwezi October wale wazee wote ambao hawawezi kutembea na ni wapiga kura wafuatwe majumbani ila wafike kwenye vituo vya wapiga kura wapige kura zao kuwachagua viongozi wao.
0 Comments