Header Ads Widget

MAPOROMOKO YA ARDHI YAUA 1000 SUDAN MMOJA ANUSURIKA

 

Watu 1,000 wamefariki dunia huku mmoja akiokolewa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliotokea katika eneo la Darfur nchini Sudan.

Maafa hayo yanatokea wakati Taifa hilo lkingia mwaka wa tatu wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyopelekea  vifo vya maelfu ya watu na hali ngumu ya maisha na ukosefu wa usalama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi la waasi la The Sudan Liberation Movement/Army wanaokalia mji huo, imeelezwa kuwa Maporomoko hayo yalianzia katika eneo la milima ya Marra magharibi mwa Sudan kisha kabla ya kufunika Kijiji cha Tarasin.

Baada ya mvua kubwa iliyonyeesha mfululuzo katika eneo hilo lenye kambi za wakimbizi waliopata hifadhi ya muda.Wamesema maporomoko hayo ya udongo yaliharibu kijiji kizima katika eneo hilo lililopo Darfur magharibi mwa Sudan.

"Taarifa za awali zinaonyesha vifo vya wakazi wote wa kijiji, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu moja, na mtu mmoja tu alinusurika," imeelezwa,.

Waasi hao pia wameomba msaada kwa UN ili kukoa miili kutoka kwenye kijiji hicho kilichofunikwa na maporomoko hayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI