Header Ads Widget

MWAKITINYA AMWOMBEA KURA DK. SAMIA ITILIMA.


 


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, MNEC Musa Mwakitinya amewataka wananchi wa Jimbo la Itilima kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Mgombea Urais kupitia CCM Dk. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwaletea Maendeleo.


Aidha, Mwakitinya amewataka Wana Itilima kutobweteka bali watafute kura za Rais Dk. Samia, Mbunge (Njalu) pamoja na Madiwani wa CCM huku wakieleza mazuri yaliyotekeleza katika utawala wake uliopita.


Aliyasema hayo jana kwenye uzinduzi wa Kampeni za Jimbo la Itilima zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Nangale, ambapo alisema serikali ya CCM imetekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo kila mahali.


Amewaomba wanaCCM kumkabidhi Rais Dk. Samia miaka mitano ili aendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia kuwa tayari ameshatekeleza miradi ya Maji pamoja na ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambayo imeanza kutoa huduma.


"Nategemea kura nyingi za Dk. Samia Suluhu Hassan zitokee hapa wilaya ha Itilima sababu mnawapiga kura wengi kuliko sehemu nyingi Mkoa wa Simiyu, mpeni kura Rais Samia, mpeni kura Njalu Silanga, wapeni kura Madiwani wa CCM ili waendelee kuchapa kazi" amesema Mwakitinya.


Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amewataka wananchi kuchagua viongozi wanaotokana na CCM ili waendelee kuchapa kazi na kuwaletea Maendeleo na kuboresha upatikanaji wa huduma katika nyanja za Elimu, Afya, Maji, Umeme, Barabara, Kilimo, Mawasiliano.


Aidha Njalu amesema endapo atachaguliwa, atahakikisha anaongeza Uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi ili kuwaletea wananchi Maendeleo huku akisisitiza kuendelea kuimarisha miundombinu katika Jimbo hilo.


Njalu amewataka Wagombea Udiwani kupitia CCM kutumia Ilani ya Uchaguzi kuomba kura huku wakieleza matarajio ya serikali ya CCM katika kutekeleza Ilani hiyo ambayo imejikita kutatua kero za Wananchi.


"Nimesimama hapa kwa kujiamini kutokana na mambo mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM chini ya Dkt. Samia, tumejipanga kuleta Maendeleo...kwenye Elimu wakati tunaomba kura Shule zilikuwa chache, sasa zitaendelea kujengwa kwa kiwango kizuri" amesema Njalu.


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI