NA AMINA SAIDI, TANGA.
ZAIDI ya vijana 1000 wenye umri wa miaka 11hadi 35 katika kata 27 za Halmashauri ya jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mradi wa "Kijana Togora, tuna kusikiliza.
Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Afya Check chini ya shirika la Tanga yetu kwa lengo la kuwafikia vijana hao na kuwapa jukwaa la kusikilizwa
Dkt. Isaac Maro, Mkurugenzi wa Afya Check na msimamizi wa mradi wa 'Kijana Togora,tuna kusikiliza "amesema kuwa mradi huo unalenga kusikiliza changamoto za maisha ya vijana Jijini Tanga kufuatia utafiti wa kina.
Sambamba na hayo Dkt Maro alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika kituo cha Sayansi cha STEMPark jijini Tanga, Aliongeza kuwa baada ya utafiti iliyobainisha changamoto nyingi wameona ni vyema kuweka utaratibu maalum wa kuwasikiliza vijana ili kujua shida zao na kuzitatua.
Mradi wa Kijana Togora,tuna kusikiliza sasa unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili wazi masuala muhimu ya ya Afya ya akili afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya na vilevi.
Pia mradi huo unatekelezwa na Afya Check chini ya Programu ya Tanga yetu inayofadhili na Botnar Foundation na kusimamiwa na Innovex umeandaa programu mahususi za kutoa suluhisho kwa changamoto zilizobainishwa baada ya kuwasikiliza vijana.
Akizungumza kuhusu mradi huo Dkt Maro "alisema pongezi nyingi ziwaendee vijana wa Tanga jiji kwa kupewa jukwaa lakusikilizwa sauti zao na hatimae kuzitatua.
Kwa upande wake Dkt Hasan Mshinda ambaye ni mwakilishi wa Botner foundation ambao ndio wafadhili wa miradi ya Tanga yetu ikiwemo Kijana Togora alisema kuwa katika utafiti waliouvanya waligundua awamu ya kwanza waliona matatizo mbalimbali ilikwemo mimba za utotoni ,maturities ya Madawa ya kulevya ambayo ndio hatarisha maisha ya vijana ambao ndio nguvu kazi Taifa
Aidha alisema kuwa Mkoa wa Tanga upo kwenye ngazi ya juu kwa maturities ya Madawaska ya kulevya hivyo kupitia mpango huo wa kijana Togora tunakusikiliza watajua kwanini wanajihusisha matumizi hayo ya Madawa ya kulevya kwamba watapa elimu ya jinsi ya kuachana uraibu huo ikiwemo ushirikiano katika ngazi ya familia .
Naye Mrakibu wa polisi wilaya ya Tanga Keneth Muhangwa alisema wao kama jeshi la polisi wameanzisha pia mradi wa ngorika kwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutokomeza maturities ya Madawa ya kulevya hivyo kwani mara nyingi wao wamekuwa wakidili na matokeo ya mambo yanayotoke katika jamii.
Kwa kuona hivyo tumeona ni vyema sisi kama jeshi kuwa mradi mahususi kwa kudili utoaji wa elimu juu ya matumizi ya Madaya ya kulevya ambapo ni vyema kila kijana atoe ushirikiano ili kutimiza wajibu wake katika kutoa taarifa ya uhalifu na wahalifu badala ya kuhusika kuafanya uhalifu unaotokana matumizivya Madawa ya kulevya.
Akizungumzi mradi huo Afisa maendeleo jiji la Tanga Bi.Fatma Kinyumbi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika kituo cha sayansi Stampark iliyoko kisosora jijini Tanga aliwashukuru na kuwapongeza Botner faundation kwa miradi mbalimbali inayohusu vijana chini ya Tanga yetu.
"Mradi wa kijana Togora ni mradi Muhimu sana kwa vijana hivyo manapaswa kuchangamkia fursa za elimu ili wafikie malengo yenu hususani kupitia mradi wa kijana Togora ni vyema kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa inayotokana na mradi huo "alisema Kinyumbi
Mwisho.








0 Comments