Header Ads Widget

BODI YA PAMBA YAWATOA HOFU WAKULIMA kuhusu UPATIKANAJI WA MBEGU.

 

Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba, Thadeo Mihayo (kulia), akiwa ameambatana na Waandishi wa Habari za Pamba wakikagua Kiwanda cha kuchakata mbegu za Pamba cha Jeylong kilichopo Mkoani Shinyanga.


Na COSTANTINE MATHIAS, Shinyanga.


BODI ya Pamba nchini imewaondoa hofu wakulima wa zao hilo juu ya upatikani wa Mbegu za kupanda katika msimu wa kilimo 2025/2026, huku ikiahidi kuwa kila mmoja atafikiwa na Pembejeo hiyo muhimu kabla ya kuanza kulima. 


Aidha, imewataka wakulima kuendelea kufanya maandalizi ya mashamba ikiwemo kukata na kung'oa masalia ili kudhibiti uhamaji wa Wadudu wanaoshambulia zao hilo la kimkakati nchini. 


Haya yameelezwa na Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba, Thadeo Mihayo akiongea na waandishi wa Habari za Pamba mara baada kutembelea Kiwanda cha Jeylong kinachochakata mbegu ya Pamba kilichopo Mkoani Shinyanga. 


Mihayo amesema kuwa Kiwanda hicho kinaondoa nyuzinyuzi kwenye mbegu za Pamba ikiwa ni moja ya mchakato wa kuaanda mbegu kwenda kwa mkulima wa Pamba. 


Amesema hadi sasa Bodi ya Pamba imepeleka kiwandani hapo kuchakata kilo mil. 12 huku lengo likiwa ni kilo mil. 13 ambapo hadi sasa wamezalisha kilo Mil. 5.8 na pia kilo mil. 3.9 zimeshapelekwa kwa Wakulima. 


"Tumejipanga kusambaza mbegu mapema kabla ya mvua ili mbegu ziweze kumfikia mkulima bila usumbufu wowote, niwahakikishie Bodi ya Pamba imejipanga katika hili...makampuni yote yaliyoelekezwa kupeleka mbegu Kwa wakulima yasambaze kwa wakati" amesema Thadeo na kuongeza.


" Kampuni ambayo inachelewa, Bodi ya Pamba ina Mamlaka ya kumwondoa na kumpa mtu mwingine, wito wangu wakulima na wengine walioko kwenye mnyororo wa uzalishaji wa Pamba, niwahakikishie mbegu ni sahihi, salama na zinaota vizuri... Wazipokee, wazitunze na kuzitumia katika mashamba yao na siyo vitu vingine"


Ameongeza kuwa mbegu zinazotoka Kiwanda cha Jeylong zinahudumia wakulima wa mikoa ya Shinyanga, Katavi, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma na ukanda wa Mashariki pamoja na Mkoa wa Simiyu wilaya ya Meatu. 


Mwisho. 


Wafanya kazi wa Kiwanda cha kuchakata mbegu cha Jeylong wakifungasha mbegu za Pamba zilizotengenezwa kwa ajili ya kupandwa katika msimu wa kilimo 2025/2026.


Mitambo ya kuchakata mbegu za Pamba katika Kiwanda cha Jeylong Mkoani Shinyanga.


Mashine za kunyonyoa Mbegu ya Pamba katika Kiwanda cha jeylong Mkoani Shinyanga.



Mashine za kunyonyoa Mbegu ya Pamba katika Kiwanda cha jeylong Mkoani Shinyanga.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI