Header Ads Widget

SHULE YETU YA MEDALA INAKIMBILIWA SANA NA WAZAZI KUTOKANA NA UBORA WETU- MKUU WA SHULE

 

Na Matukio Daima Media 

Mkuu wa shule ya Medala High School Moses Mazengo amewataka wazazi na walezi kuweza kuchangamkia fursa ya kuwapeleka watoto shule katika muhula mpya wa masomo wa 2026 haswa kwa wototo wanaomaliza darasa la saba saivi.

Akizungumza na Matukio Daima Media Mazengo amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho muhula wa masomo unakaribia kumalizika wazazi wanalojukumu kubwa la kuhakikisha wanawapeleka watoto wao katika shule bora.

“Mimi nipo hapa na dhumuni moja tu la kuwatangazia wazazi na walazi waliopo mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kwamba Medala kwa sasa inapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaoanza januari 2026 lakini kabla ya januari kuna zoezi la kufanya usaili ambapo zoezi hili litafanyika siku ya tarehe 20 jumamosi na tarehe 27 mwenzi huu wa tisa katika maeneo tofautitofauti”.

Pia ameeleza kuwa shule ya Medala kwasasa watakuwa na pre form one kozi ambayo itaaanza tarehe 29 mwezi huu ambapo usaili utafanyika katika vituo mbalimbali kwaajili ya kuwaandaa watoto kwa mafunzo ya mwakani.

“Tutakuwa na pre form one kozi ambayo itaanza mwezi huu tarehe 29 ambapo kwa mkoa wa Iringa usaili utafanyikia katika Chuo cha ualimu Kleruu lakini kwa wale wa kazi wa Dar es Salaam usaili utafanyikia pale Msimbazi Center na muda wa kufika ni saa mbili asubuhi hiyo siku ya jumamosi”

Aidha ameelezea mwitikio wa wazazi katika kipindi hiki  katika kuwaleta watoto shuleni huku akiongeza kuwa nafasi bado zipo kwa wazazi na walezi ambao wanahitaji kuwaleta watoto wao. 


”Mwitikio ni mkubwa na tunadhani kwamba wale ambao wamechelewa pengine wawahi kwa siku mbili tatu hizi kwasababu kuna uwezekeno nafasi zikaisha na wale ambao wanatamani kuwaleta watoto Medala wakakosa nafasi, kwaio niwahimize wale ambao wanawiwa kuweza kuwaleta watoto basi wajitahidi inapofika tarehe 27 wawe tayari wameshachukua fomu kabla dirisha halijafungwa”.

Pia Mazengo ameelezea umuhimu wa matangazo ambayo kwa kiasi kikubwa yamesaidia shule ya Medala kuweza kufahamika kwa ukubwa ukilinganisha na kipindi ambacho bado haijatangazwa

“Kwa ujumla mwanzoni shule yetu ilikuwa haijulikani lakini katika miaka hii miwili tangu tumeanza kuona matangazo ya Matukio Daima Media yakirushwa katika mitandao mbalimbali tunaona mwitikio na watu wanaielewa na tunashukuru kwasababu hata idadi ya wanafunzi imeogezeka’’. 

Hatahivyo ameongeza kuwa wao kama shule wanawahakikishia wazazi na walezi kuwa shule hiyo ya Medala ipo kwaajili ya kuwahudumia wanafunzi.

Aidha Mazengo amejibu swali la kwanini Medala ni shule bora kwa mzazi kuweza kumpeleka mwanao.

“Ukiona kitu kinazungumzwa sana basi ujue kina ubora wake na ubora wa Medala upo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mazingira ya shule ambayo yanapendeza wakati wote lakini pia miundombinu ambapo tuna majengo ya kisasa na ukiachilia hayo yote ni huduma ambazo wanazipata watoto haswa upande wa chakula lakini kubwa zaidi ni ufaulu mzuri wa wanafunzi ukiangalia matokeo yetu ya 2024 yanadhihirisha kwamba tunasogea na tunafanya vizuri” 

Shule ya Sekondari ya Medala ni shule ya Private iliyopo  katika mkoa wa Iringa, wilaya ya Iringa, kijiji cha Idodi karibu na Mbuga ya wanyama Ruaha National Park.


FOMU ZA KUJIUNGA NA MEDALA BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI