Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp
MASHINDANO ya mbio za magari, African Rally championship kwa mara ya kwanza mkoani Morogoro yanatarajiwa kuanza sept. 19 hadi 21 mwaka huu 2025, ambapo hadi sasa washiriki 23 wameshajiandikisha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo msimamizi mkuu wa mashindano hayo Dk. Mosi Makau amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 95.
Aidha Dk. Makau amesema maeneo yatakayotumika katika mashindano hayo ni shamba la miti la TFS na shamba la mkonge Tungi Manispaa ya Morogoro.
Hata hivyo Dk. Makau alisema kuwa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo ya magari ni madereva wenye uwezo mkubwa zaidi na wanawania taji la Afrika.
kwa upande wake mwakilishi kutoka Mkwawa Leaf ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo Emanuel Mhagama alisema kuwa kampuni yao inashirikiana na serikali kupitia wizara ya utamaduni sanaa na michezo katika kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mafanikio.
Hata hivyo Mhagama alisema kuwa mashindano hayo yanawashirikisha washiriki wenye uzoefu mkubwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda, Kenya, India na Burundi.
Aidha amesisitiza kuwa wao kama kampuni wako tayari kushirikiana ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha juu.





0 Comments