Header Ads Widget

DK. NCHIMBI AWAOMBEA KURA DK. SAMIA, NJALU NA MADIWANI, ITILIMA.

 



Na COSTANTINE MATHIAS, Matukio Daima app.


MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi amewaomba wananchi wa Jimbo la Itilima Mkoani Simiyu, kuwapa kura za ndio Mgombea Urais  Dk. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Njalu Silanga pamoja na Madiwani.


Akizungumza leo kwenye Mkutano wa kampeni, katika viwanja vya Stendi ya Langangabilili wilayani humo, amesema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali ya Dk. Samia imefanya Maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa Madaraja 52 kutoka 12 ya awali na ujenzi wa Barabara zaidi ya kilometa 800 kutoka kilometa 500.


Awali, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Njalu Silanga (CCM), amesema Utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa Vitendo ndio sababu kubwa iliyowapa Imani wananchi ya kuendelea kukiamini Chama hicho, jambo lililosababisha Madiwani 19 kati ya 22 kutokuwa na wapinzani.


Aidha, Mgombea huyo wa Ubunge (Njalu) ameongeza kuwa Halmashauri ya wilaya ya Itilima imepokea zaidi ya shilingi Bil. 92kKwa ajili ya mbalimbali ya Maendeleo na kisha kuwashukuru wanachama na wapenzi wa CCM kwa mshikamano.


Mwisho.













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI