Na WILLIUM PAUL, SAME.
MBUNGE mteuli wa viti maalum kupitia chama cha Mainduzi mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amewataka wananchi kuepuka kudanganyika na Wasanii wa siasa ambao wamekuwa wakieneza maneno ya uongo kwao na badala yake kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo kutoka ndani ya ccm.
Zuena alitoa kauli hiyo leo katika uzinduzi wa kampeni za Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecel katika kata ya Maore ambapo alisema wapo wanasiasa ambao ni Wasanii kazi yao kueneza uongo ili waweze kuchaguliwa.
"Wapo Wasanii wa siasa ambao wamekuwa wakipita na kuwatapeli wananchi ili muweze kuwachagua wakati hawawezi hata kuongoza, wao wenyewe na vyama vyao wamekuwa wakiparangana sasa mnapaswa kutambua ccm ndio chama kinachoweza kuwaletea maendeleo" Alisema Zuena.
Mbunge huyo aliwataka Wananchi kumchagua Anna Kilango kwani ni mbunge ambaye anaweza kusemea Jimbo lake na kuwaletea wananchi maendeleo ambapo amekuwa akipambana Bungeni kuhakikisha miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo inasonga mbele.
"Tuna tambua katika kura za maoni kila mtu alikuwa na mtu wake lakini sasa tumeshapata Rais, Mbunge na Madiwani sasa tunapaswa kuvunja makundi na kwenda na wagombea wa ccm na maendeleo ya kweli ni Samia Suluhu Hassan na Anna Kilango pamoja na Madiwani wa ccm wengine wapuuzenu hawawezi kuwaletea maendeleo" Alisema Zuena.
Mwisho.
0 Comments