Header Ads Widget

BODI YA KOROSHO TANZANIA CBT YAANZA MAANDALIZI YA MSIMU WA KOROSHO KWA MAFUNZO YA UBORA WA KOROSHO KUANZIA SHAMBANI

 

Bodi ya Korosho Tanzania CBT imeanza maandalizi ya mauzo ya zao la Korosho kwa kutoa Mafunzo kwa Maafisa Ugani na Maafisa Kilimo wa Wilaya ya Mkuranga kuelekea msimu mpya wa mauzo ya zao la Korosho kwa mwaka 2025/2026.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja WA Bodi ya Korosho Tanzania tawi la Dar es Salaam na Pwani BI. Domina Mkangala wakati Mafunzo kwa Maafisa Ugani na Maafisa Kilimo wa Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya WA mauzo ya zao la Korosho kwa mwaka 2025/2026.

Amesema mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya 
Utafiti ya Kilimo nchini TARI Naliendele wameendesha mafunzo ya ubora wa Korosho kuanzia ngazi ya mkulima shambani katika mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga.

Domina alisema mafunzo hayo ni mwendelezo kwa wakulima wa Wilaya zote za mkoa wa Pwani ambapo Maafisa Ugani na Maafisa Kilimo 

"Bodi ya Korosho kupitia tawi lake la Dar es Salaam na Pwani imeendesha mafunzo ya ubora wa korosho kwa wataalamu wa kilimo, ugavi na maafisa wa mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora kwa Sekta ya Korosho, maarufu kama NOTA, katika wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani" alisema Domina.

"Mafunzo hayo yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa wataalamu hao kwa ajili ya msimu mpya wa mauzo ya korosho wa mwaka 2025/2026. Hili ni sehemu ya muendelezo wa mafunzo yanayoendeshwa katika wilaya zote za mkoa wa Pwani" alisema.

Kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kituo cha Naliendele, Bodi ya Korosho inalenga kuhakikisha wataalamu wanapata elimu ya kina kuanzia hatua ya awali ya uzalishaji wa korosho, yaani shambani, hadi hatua ya mwisho ya uhifadhi katika maghala ya vyama vya msingi.
 
Domina Mkangala alisema kuwa mafunzo haya yanahusisha matumizi sahihi ya viuatilifu, mbinu bora za uvunaji, na njia salama za uhifadhi wa korosho.


"Lengo letu ni kuhakikisha wataalamu wetu wanawafikia wakulima na kuwapatia maarifa sahihi ya namna bora ya kuvuna, kuhifadhi na kusafirisha korosho hadi kwenye maghala ya vyama vya msingi. Hii itasaidia kuongeza ubora wa zao la korosho na kuimarisha ushindani wake katika soko la dunia," alisema Bi. Mkangala.

Aidha, aliongeza kuwa dhamira ya mafunzo haya ni kuhakikisha kwamba korosho zote zinazozalishwa katika mkoa wa Pwani na maeneo mengine nchini zinakuwa katika daraja la kwanza kwa ubora, lengo likiwa kufikia asilimia 98 ya korosho bora zinazotoka Tanzania.

Kwa maelezo yake, mafunzo haya yanatazamiwa kuwa kichocheo kikubwa cha kuinua tija kwa wakulima na kusaidia juhudi za kitaifa za kulinda na kuinua thamani ya korosho za Tanzania katika masoko ya kimataifa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI