Header Ads Widget

MASHTAKA YA MAUAJI NA UHAINI DHIDI RIEK MACHAR NI 'HUJUMA ZA KISIASA' -UPINZANI SUDAN KUSINI

 

Upinzani wa Sudan Kusini umeuuzilia mbali mashtaka ya uhaini na mauaji dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Riek Machar ukiyataja kama "fitina za kisiasa" zinazotishia makubaliano dhaifu ya amani ya nchi hiyo.

Kaimu Mwenyekiti wa SPLM-IO, Nathaniel Oyet, ameiambia BBC mashtaka kuwa hayo ni ukiukaji wa moja kwa moja wa makubaliano ya amani ya 2018.

"Hili ni pigo kwa wadhamini wa makubaliano ya amani yaliyofufuliwa, na pigo kubwa sana kwa mchakato wa amani katika Jamhuri ya Sudan Kusini," alisema. Oyet alimuonya Rais Salva Kiir kuwa hana mamlaka ya kumsimamisha kazi Machar, na kuongeza kuwa : "Jaribio lolote la kufanya hivyo, litamaanisha kuwa Rais pia anajisimamisha kazi."

Kaimu Katibu wahabari wa Machar Puok Both Baluang, aliishutumu serikali kwa kutunga kesi hiyo.

"Shutuma hizo ni fitina za kisiasa, zilizoratibiwa na Salva Kiir na washirika wake, walioshirikiana kuvunja makubaliano ya amani," amesema.

Alitupilia mbali kesi hiyo akiitaja kuwa isiyo na msingi, akidai mahakama "haina uhuru, badala yake inafanya kazi kama mahakama zinazoongozwa kisiasa."

Nae Reath Muoch Tang, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya mahusiano ya kigeni ya SPLM-IO, ameyaita mashtaka hayo "yaliyotengenezwa na SPLM-IG katika jaribio la makusudi la kubatilisha makubaliano ya amani na kuimarisha utawala wa kimabavu wa kabila moja."

Aliongeza: "Kitendo chenyewe cha kutangaza hadharani mashtaka haya ni uingiliaji wa kisiasa na kuathiri mchakato wa mahakama."

Viongozi wa upinzani pia walikanusha madai ya serikali yanayomhusisha Machar na shambulio baya la Machi huko Nasir, ambapo zaidi ya wanajeshi 250 na rubani wa Umoja wa Mataifa waliuawa.

Wizara ya Sheria ya Sudan Kusini imetetea uamuzi wake, ikisisitiza kuwa wale waliohusika na ukatili "watawajibishwa, bila kujali nafasi zao au ushawishi wao wa kisiasa."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI