Na Matukio daima media
Mgombea Ubunge Jimbo la Karagwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Innocent Bashungwa, ameendelea na mikutano ya kampeni zake katika Kijiji cha Kanogo, Kata ya Nyakabanga, Wilaya ya Karagwe.
Katika mkutano huo, Bashungwa ameahidi wananchi huduma ya maji safi kwa kuchimba visima kupitia mitambo ya Wizara ya Maji ambapi ameweka bayana dhamira ya Serikali ya kufikisha umeme katika vitongoji vyote vya kijiji hicho ili kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.
Bashungwa amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 kwa kujitokeza kwa wingi na kuwachagua kwa kishindo Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge pamoja na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi ili kuendeleza maendeleo ya Taifa.
Kampeni hizo zinazofanyika ngazi ya vijiji zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Karagwe, Paschal Rwamugata.





0 Comments