Na Matukio Daima Media
KANISA katoliki Jimbo la Mafinga limetolea ufafanuzi tukio la Padre Jordan Kibiki aliyedaiwa kujiteka kuwa anatatizo la afya ya akili na sasa polisi wamemwachia huru baada ya kubaini ukweli huo .
"Padre Kibiki ambae ni mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Nyololo na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Nyololo baada ya kuibuka kadhia aliyokutana nayo kuanzia Septemba 18 Septemba 2025 "
kuwa Septemba 18 mwaka huu 2025, Padre Jordan alitarajiwa kuhudhuria kikao cha mambo ya afya katika Ofisi za Halmashauri ya Mufindi, lakini alishindwa kufika licha ya kuondoka mapema asubuhi.
Alisema kuwa Padre Isaac Nzigilwa, Paroko wa Parokia ya Nyololo, alipokuwa akisafiri kutoka Mafinga aliona gari la Padre Jordan lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara, na alijaribu kuwasiliana naye, akidhani kuwa alikuwa salama.
Hata hivyo alisema Padre Jordan hakurudi nyumbani kwa muda mrefu na juhudi za kutafuta zilianza baada ya kuripotiwa kuwa hakufika Kituo cha Afya.
Baada ya masaa kadhaa ya kutafuta, gari la Padre Jordan lilionekana tena, na baada ya uchunguzi wa awali, ilibainika kuwa alikuwa amejiweka katika hali ya kutokuwa na utulivu (depression).
"Alienda kutafuta msaada, na katika mahojiano na Jeshi la Polisi, Padre Jordan alieleza kuwa alikubaliana na wizi wa fedha alizokuwa amekopa, na kwamba hali hiyo ilikuwa imemwingiza katika hali ya kifurugha na hofu kubwa"
Kuwa baada ya kufuatilia tukio hilo kwa karibu na kushirikiana na vyombo vya uchunguzi, Jeshi la Polisi lilithibitisha kuwa Padre Jordan alikuwa hajatekwa kama alivyodai awali, bali alijitokeza mwenyewe.
Hata hivyo, kutokana na hali yake ya kiakili, uchunguzi wa matibabu ulithibitisha kuwa alikuwa akihisi huzuni na maumivu kutokana na hasara ya kifedha aliyopata kupitia biashara ya mtandao.
Alisema kuwa hali hiyo ilipelekea Padre Jordan kuwekwa chini ya uangalizi wa kisheria, na baadaye alijikuta katika hali ya kuponya afya yake baada ya kupelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Tosamganga.
kuwa hadi Septemba Septemba 2025, Jeshi la Polisi lilifuta tuhuma dhidi ya Padre Jordan, na aliachiliwa huru.
"Tunaelewa kuwa kwa mujibu wa sheria za Kanisa, masuala ya kibinafsi ya Padre yanahitaji kushughulikiwa na yeye mwenyewe, na Kanisa halihusiki moja kwa moja katika masuala hayo, lakini tunatoa wito kwa jamii kuendelea kumwombea Padre Jordan kwa ajili ya kupona kwake".
Alisema kuwa wanaendelea kushughulikia afya ya Padre Jordan, na lengo ni kumsaidia kurejea kwenye hali ya utulivu na kuendelea na huduma yake ya kiroho.
"Tunatoa shukrani kwa vyombo vya habari kwa kushirikiana nasi katika kipindi hiki kigumu, na tunawataka wote kuendelea kueneza upendo, amani na haki katika jamii"alisema askofu Mwagala
0 Comments