Na mwandishi wetu
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza ratiba ya uchukuaji wa fomu za kugombea urais, uwakilishi na madiwani. Zoezi hilo litafunguliwa na Chama cha Mapinduzi Agosti 30, Licha ya ratiba ya uchukuaji wa fomu kuanza leo, nafasi ya urais itaanza kuchukuliwa Agosti 30.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Zanzibar, Thabit Idarous Faina amesema kuwa tume hiyo inatarajia kutumia shilingi bilioni 12 kwa maandalizi yote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Aidha Kwa mujibu wa ratiba, CCM itafungua dimba saa 4:00 asubuhi, kikifuatiwa na NLD saa 5:00 asubuhi, AAFP saa 6:00 mchana, CUF saa 7:00 mchana, na TLP saa 8:00 mchana kabla ya NRA kufunga siku hiyo saa 9:00 alasiri.”
Pia kwa siku inayofuata, Agosti 31, NCCR Mageuzi kitakuwa cha kwanza saa 3:00 asubuhi, ACT-Wazalendo saa 4:00 asubuhi, CCK saa 5:00 asubuhi na DP saa 6:00 mchana. ZEC imesisitiza kuwa vyama vyote lazima viwe na namba maalum ya malipo kabla ya kuchukua fomu, na tayari vyama vyote 17 vimeshakamilisha utaratibu huo.
0 Comments