Header Ads Widget

MAADHIMISHO YA MIAKA 64 YA MAGEREZA YANG’ARA MOROGORO

Morogoro imekuwa moja ya mikoa iliyoshuhudia upekee wa maadhimisho ya miaka 64 ya Jeshi la Magereza, ambapo askari na maafisa wa magereza wameshiriki kwa vitendo kwenye shughuli za kijamii.

Kwa pamoja wamefanya usafi katika kituo cha afya Sabasaba, wakachangia damu na kupeleka msaada kwa makundi yenye uhitaji.

 Mkuu wa Magereza Mkoa, SACP Petter Laurian Anatory, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu inayosisitiza mshikamano kati ya magereza na jamii kwa ajili ya urekebishaji wenye tija.

Matukio Daima imeshuhudia Askari na maafisa kutoka Gereza la Kihonda, Gereza la Mahabusu Morogoro na Askari na maafisa kutoka ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wakishiriki kufyeka, kuokota na kuzoa taka, kudeki, kutengenezea maua kwenye kituo cha afya cha manispaa ya Morogoro  cha Sabasaba.

Mkuu wa gereza hilo, SSP Nicostratus Magori, alisema miradi hiyo inawasaidia wafungwa kupata ujuzi utakaowasaidia baada ya kumaliza vifungo vyao.

Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni pamoja na kituo cha watoto yatima na wenye mahitaji maalum cha Mgolole na kituo cha wazee wasiojiweza cha Mgolole vilivyopo Kata ya Bingwa manispaa ya Morogoro.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI