Mahakama Kuu ya Tanzania leo inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua inayoweza kubadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kesi hiyo imepewa kipaumbele kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa na chama hicho, kikidai kuwa uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wa kumvua Mpina haki ya kugombea, ni kinyume cha sheria na haki za kidemokrasia.
Kwa mujibu wa mawakili wa ACT-Wazalendo, mahakama leo itasikiliza hoja za awali zitakazobainisha iwapo zuio hilo lilikuwa halali kisheria au ni uamuzi wa kiutendaji uliopita mipaka ya kikatiba.
Iwapo Mpina ataibuka mshindi katika shauri hili, atarejeshwa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha urais, hatua ambayo inaweza kuongeza ushindani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
0 Comments