Header Ads Widget

WANU NA MASAUNI WAVUNJA REKODI ZANZIBAR,VINARA KURA ZA MAONI UBUNGE ZANZIBAR

Aliyekua Mbunge Viti Maalum Wanu Hafidh Ameir na aliyekua Mbunge wa Jimbo ka Kikwajuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni wanaangaziwa kuongoza wagombea wote waliopigiwa kura za maoni CCM kwa nafasi ya Ubunge katika Majimbo 50 ya Zanzibar 

Wanu akichukua nafasi ya kwanza ametangazwa kuongoza kura za Maoni kwa kupata kura 1356 akimuacha mpinzani wake wa nafasi ya pili aliyepata kura 03 tu

Nafasi ya pili ikibebwa na Masauni aliyetangazwa kuongoza kura za maoni kwa nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Kikwajuni Zanzibar kwa kupata kura 790 huku mpinzani wake wa nafasi  ya pili ambae ni mtoto wa Familia ya Mzee Karume, Said Ali Karume akiambulia kura 50 tu

Katika takwimu hizo anashikilia nafasi ya tatu ni Makame Mbarawe aliyetangazwa kuongoza kura za Maoni kwa nafasi ya ubunge jimbo la Mkoani Pemba kwa kupata kura 693

Kutokana na takwimu za wagombea Zanzibar katika mchakato wa kura za Maoni, watatu hao wanatajwa kuwa vinara wa kuzoa kura nyingi na kuwaacha wapinzani wao kwa kura chache sana ukilinganisha na wagombea wengine waliongoza nafasi hiyo katika Majimbo ya Zanzibar na kuingia katika rekodi mpya ya medali za siasa na Uongozi

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI