Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAPATIWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.



Na Editha Karlo,Kigoma
WAANDISHI wa habari wa Mkoa wa Kigoma wamepewa mafunzo usalama na ulinzi wa kimwili na kidigitali na afya ya akili katika kipindi hiki muhimu tunachoelekea uchaguzi mkuu octoba 29 mwaka huu.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamefanyika katika ofisi za chama cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma(KGPC)na kushirikikisha baadhi ya waandishi toka vyombo mbalimbali Mkoani humo Katibu wa chama cha waandishi Mkoa wa Kigoma (KGPC)Mwajabu Hoza alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yamekuja wakati sahihi.


Baadhi wa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza mkufunzi Adela Madyane wakati akitoa mada ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa Mkoa wa Kigoma

"Nina waomba waandisi wenzangu tuzingatie haya mafunzo tutakayifundishwa leo na wakufunzi wetu kwani haya ni mafunzo muhimu kwetu na yamekuja kwa wakati sahihi ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu octoba mwaka huu"alisema Mwajabu

Katibu Mwajabu alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa"Empowering journalist for infurmed community"unaofadhiliwa na umoja wa ulaya(EU)na shirika la maendeleo la uswisi(SDC).

mkufunzi Izack Aron akitoa mada ya usalama mitandaoni kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa kigoma

lisema pia mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa International Media Support(IMS)Union of Tanzania press Club(UTPC)pamoja na jamii Africa.

"Hawa wakufunzi wetu wa leo ni waandishi wenzetu ambao walijengewe uwezo na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)na kisha kutakiwa waje kutujengea uwezo na sisi ili tuwe salama kupitia mafunzo haya watakayotupa leo"aliongeza kwa kusema pia


waandishi wakifuatilia mada kwa makini zinazotolewa na wakufunzi kwenye mafunzo ya usalama na ulinzi kwa waandishi wa habari

Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Adela Madyane ambaye ni mwandishi wa habari akitoa mada ya ulinzi na usalama alisema waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi kwa kujilinda wakati wote kwani ulinzi na usalama huanzia kwa mwandishi mwenyewe.

Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Izack Aron ambaye ni mwandishi wa habari akitoa mada ya usalama mitandaoni aliwataka waandishi kuzingatia umuhimu wa kuweka nywila imara katika vifaa vyao vya kazi na kuepuka kubofya viunganishi visivyo salama mitandaoni.
"Tuwe makini tunapotumia mitandao mambo ya kupenda kujiunda wifi za bure tuache utajikuta taarifa zako zinadukuliwa bila wewe kujua,pia tuache tabia ya kubofya viunganishi ovyo vingine vinakuwa siyo salama tunapaswa kuwa na nywila imara katika vifaa vyetu vya kazi"alisema Izack

Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo Emanuel Matinde wa Clouds TV,Emanuel Sennywa Radio Joy na Nyankolema Mwita wamesema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo na wamejua jinsi ya kufanya kazi kwa kwa kujilinda kuanzia wao hadi vifaa vyao vya kazi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI