Rais Donald Trump, aliyekerwa na kauli za Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev, anasema ameamuru manowari mbili za nyuklia kusogea karibu na Urusi.
Kwa hivyo, Moscow itajibuje? Je! tuko kwenye njia ya mzozo wa nyuklia kati ya Marekani na Urusi?
Vyombo vya habari vya Urusi vimepuuza tangazo la Trump.
Akizungumza na gazeti la Moskovsky Komsomolets, mchambuzi wa masuala ya kijeshi alihitimisha kuwa Trump alizungumza "akiwa na hasira". Luteni jenerali mstaafu aliiambia Kommersant kwamba mazungumzo ya rais wa Marekani kuhusu manowari yalikuwa "makelele yasiyo na maana". "Nina hakika Trump hakutoa maagizo yoyote [kuhusu manowari]," mtaalam wa usalama wa Urusi alisema.
Kommersant pia anataja kwamba mnamo 2017, Trump alisema kwamba alituma manowari mbili za nyuklia kwenye peninsula ya Korea kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Hata hivyo muda si mrefu, Trump alifanya mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kwa hivyo, cha ajabu, je, kupelekwa kwa manowari ya hivi punde zaidi ya Donald Trump kunaweza kuwa utangulizi wa mkutano wa kilele wa Marekani na Urusi?
0 Comments