Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
MGOMBEA urais kupitia chama cha United Peoples' Democratic Party (UPDP), Twalibu Kadege, amefanikiwa kuchukua fomu ya uteuzi ya kugombea urais pamoja na mgombea mwenza wake.
Akizungumza leo Agosti 10 2025 mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi ya Taifa ya Uchaguzi INEC, Kadege amesema kuwa kwa sasa hana mengi ya kueleza kwa kuwa ilani ya chama haijazinduliwa rasmi, ingawa amebainisha kuwa sera kuu ya chama hicho ni kuhusu ardhi.
Akiambatana na mgombea mwenza, Abdallah Mohamed Khamis, ameeleza kuwa ardhi ikitumiwa vizuri itawanufaisha wananchi, lakini ikitumiwa vibaya haitawanufaisha Watanzania.
Ameongeza kuwa watajikita katika kushughulikia sekta ya kilimo na afya, huku wakijipanga kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri ya huduma za afya.
Vilevile, ameahidi kuwa katika ilani ya chama, waandishi wa habari watawezeshwa kupata vifaa muhimu ili waweze kuripoti habari hata wakiwa vijijini bila kubughudhiwa.
Mwisho
0 Comments