Header Ads Widget

TUNAMPELEKA BUNGENI BABA LEVO : KILUMBE NG'ENDA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuia ya wazazi CCM Taifa Kilumbe Ng’enda amesema kuwa wamejiandaa kuhakikisha mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini kupitia CCM  Clayton Revocatus Chipando Maarufu Baba Levo anaingia bungeni kwa kushindaa ubunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.

Ng’enda alisema hayo akiongea na viongozi na wanachama wa CCM ofisi kuu ya CCM mkoa Kigoma  alipowasili mkoani Kigoma kwa mapumziko mafupi baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Jumuia ya wazazi  CCM Taifa baada ya kukatwa kugombea jimbo hilo licha ya kuongoza kwenye kura za maoni.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Jumuia ya wazazi alisema kuwa chama kimeamua kumpitisha Baba Levo hivyo ni lazima viongozi na wanachama wote kuheshimu uamuzi huo lakini kumuunga mkono Mgombea huyo ambaye kwa sasa anapambana na Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Pamoja na kusimamia kura za Baba Levo Naibu Katibu Mkuu huyo wa jumuia ya wazazi alisema kuwa watahakikisha wanasimaamia kura za Mgombea uraisi wa Chama hicho, Samia Suluhu Hassan, wabunge wote wa mkoa huo na madiwani na kutaka wana CCM kuungana kwa nguzu zote kuhakikisha chama hicho kina shinda kwa kishindo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI