Rais wa Marekani Donald Trump anasema ameamuru manowari mbili za nyuklia "kuwekwa katika maeneo yanayofaa" kujibu matamshi "ya uchochezi" ya Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev.
Trump alisema alitenda hilo "ikiwa tu kauli hizi za kipumbavu na za uchochezi ni zaidi ya hayo. Maneno ni muhimu sana, na mara nyingi yanaweza kusababisha matokeo yasiyotarajiwa, natumai hili halitakuwa mojawapo ya matukio hayo".
Hakusema ni wapi manowari hizo mbili zilikuwa zikipelekwa, kwa kuzingatia itifaki ya kijeshi ya Marekani.
Medvedev hivi karibuni ameitishia Marekani kujibu matamshi ya Trump kwa Moscow ya kukubali kusitisha mapigano nchini Ukraine, la sivyo itakabiliwa na vikwazo vikali.
Urusi na Marekani zinamiliki silaha nyingi zaidi za nyuklia duniani, na nchi zote mbili zina kundi la manowari za nyuklia.
Katika chapisho la Ijumaa, Trump aliandika: "Kulingana na matamshi ya uchochezi ya rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev, ambaye sasa ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, nimeamuru manowari mbili za nyuklia ziwekwe katika maeneo yanayofaa".
Rais wa Marekani hakusema iwapo alikuwa anarejelea manowari zinazotumia nguvu za nyuklia.
Akizungumza na waandishi wa habari baadaye siku ya Ijumaa, Trump alisema: "Tishio lilitolewa, na hatukufikiri kuwa linafaa. Kwa hivyo lazima niwe makini sana.
0 Comments