Header Ads Widget

SUA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

 


Na Lilian Kasenene, Morogoro

Matukio DaimaApp 

CHUO Kikuu cha Sokoni Cha Kilimo(SUA) kimeibuka kidedea kwa kupata ushindi wa jumla na ushindi wa kwanza kwa taasisi za mafunzo na utafiti katka maonesho ya wakulima,Wafugaji na wavuvi Kanda ya mashariki yaliyohitimishwa kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Morogoro.


Maonesho hayo ya Kilimo Nanenane Kanda ya Mashariki yalionyesha teknolojia za kisasa za kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wenye tija, uvuvi wa kisasa pamoja na usindikaji na uchakataji wa mazao kwa viwango vya juu.


Ushindi huo ni juhudi za pamoja kati ya wadau wa SUA, Wafanyakazi na wanafunzi, katika kuandaa na kuwasilisha bunifu,tafiti na teknolojia zinazochangia Maendeleo ya Kilimo nchini.

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokine Cha Kilimo SUA Prof Raphael Chibunda akipokea kombe la mshindi wa jumla nanenane Kanda ya mashariki


Akiahirisha maonesho hayo mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Buriani alisema mabadiliko hayo ni matokeo ya uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025” inafundisha umuhimu wa kuwa na viongozi wanaochochea maendeleo na kushughulikia changamoto kwa ufanisi.


Alisema kupitia jukwaa la business to business, wakulima, wafugaji, wavuvi na maafisa ughani wamepata mafunzo ya mnyororo wa thamani, masoko, ufungashaji, fursa za kifedha na matumizi ya teknolojia, huku kuwaleta pamoja watafiti, wazalishaji na wanunuzi kukiwa ni daraja la mageuzi ya kilimo.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, alisema maonesho hayo yatakuwa endelevu baada ya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya maji yanayopatikana saa 24, na eneo hilo la Nanenane.


Alisema uwanja huo utakuwa ni soko endelevu la mbogamboga kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ambapo aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kupata huduma.


Aidha Malima alisema sambamba na hatua hiyo, kutakuwa na mpango wa kuufanya uwanja huo kuwa kituo cha burudani na maonesho ya wanyama hai.


Mabanda mengine yaliyoshinda ni Jeshi la kujenga Taifa(JKT), Jeshi la Magereza, Shirika la hifafhi za Taifa(TANAPA) na baadhi ya Halmashauri za Wilaya za Mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga na Dar es salaam ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, na Mlimba,


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI