Header Ads Widget

SHILATU AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJI

 


~ Wampokea kwa shangwe kubwa

~ Ni ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Madereva Bodaboda na Bajaji.

Na Matukio daima media

Waendesha Bodaboda na Bajaji wamempokea kwa shangwe kubwa Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu kwenye ziara yake ya kutembelea Kata kwa Kata kusikiliza na kutatua kero za Waendesha Bodaboda na Bajaji.

Shilatu alikutana na kufanya nao vikao na mikutano waendesha Pikipiki hao maarufu kama Bodaboda kuzungumzia utendaji kazi wao, hali ya ulinzi na Usalama pamoja na kuwahimiza kushiriki uchaguzi Mkuu wa kumchagua Diwani, Mbunge na Rais kwa amani na utulivu.

Kwenye ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana pamoja na Kamati ya Usalama ya Tarafa ambapo msisitizo mkubwa ni utii wa Sheria bila shurti pamoja na kulinda amani na Usalama.

"Tumekuja hapa kuwakumbusha juu ya umuhimu kuzijua na kuzitii Sheria za Usalama barabarani na pia kuendelea kuimarisha mahusiano zaidi kati yenu na Jeshi la Polisi na Serikali ambayo nyakati zote mmkekuwa mkitoa ushirikiano. Lakini pia kuwasisitiza zaidi kushiriki uchaguzi Mkuu huu kwa amani na utulivu huku mkiendelea kuimarisha ulinzi na Usalama kwenye wa nchi." Alisisitiza Gavana Shilatu.
Akizungumza kwa niaba ya Waendesha Bodaboda na Bajaji, Dan Bonge amesema wamefurahishwa na ziara hiyo kwani haijawahi kutokea Kiongozi mkubwa kuwafuata kwenye maeneo yao ili kuziona, kuzitambua na kushughulikia kero zao kwa muda mrefu huku akisisitiza wataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali iliyopo Madarakani na kuomba ikiwezekana Serikali iendelee kuwapatia mikopo ili wajiimarishe zaidi kwenye kazi zao za udereva Bodaboda na Bajaji.


Akijibu hoja ya Mikopo Afisa Maendeleo ya Kata ya Lukuledi, Ndugu Musa Soud aliwahakikisha Madereva hao kushirikiano nao kwenye hatua zote ili waendelee kuwapata mikopo ya Halmashauri huku Gavana Shilatu akihaidi kufuatilia suala hilo la mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri ili nao wawe sehemu endelevu ya wanufaika huku akiwakumbusha wasisahu kurejesha mikopo hiyo ndani ya muda unaotakiwa baada ya kupatiwa.



Shilatu pia alimpongeza Dereva Bodaboda wa pekee Mwanamke na kuwahimiza Wanawake wengineo kuiga mfano huo wa kufanya kazi pasipo kuchagua wala kubagua kazi kwani Mwanamke pia anaweza kufanya kazi sawa na Mwanaume.

Kwenye ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana pamoja na Kamati ya Usalama ya Tarafa, Wataalamu ngazi za Kata, viongozi wa vijiji kwenye ziara hiyo ya kusikiliza na kutatua kero za Waendesha Bodaboda na Bajaji Kata kwa Kata.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI