Na Fatma Ally Matukio Daima
Rais wa Shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) Rajab Amiry leo amerudi nchini Tanzania akitokea nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Botswana, Ethiopia na South Afrika lengo ni kujifunza na kushirikiana na viongozi wa mashirikisho wa Filamu barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agost 10, 2025, mashirikisho ya filamu barani Afrika yamelenga kuandaa chombo kimoja maalum kitakachotumika kuonesha kazi za wasanii wa Filam kutoka mataifa yote ya Afrika.
Amesema kuwa, mazungumzo yao katika ziara hiyo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kisekta, kuongeza nasoko ya kazi za wasanii na kuanzisha majukwaa ya pamoja ya maonyesho ya filamu za kiafrika.
Aidha, amesema Shirikisho la filamu Tanzania limeahidi kutoa Taarifa za kina kuhusu hatua zitakazofuata ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa chombo cha pamoja na maonyesho ya filamu za Afrika.
Katika hatua nyengine amesema alichukua fomu ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa Jimbo la Segerea, aligundua changamoto kadhaa ikiwemo huduma za Afya hususani kwa wazee ambapo ameahidi kila mtaa atamchukua mzee mmoja na kugharamikia miwani .
Ameongeza kuwa wakati wa kampeni umekwisha kiongozi yoyote atakae tangazwa ni wajibu wananchi kumpokea huku kuahidi kutoa ushirikiano kwani changamoto za Jimbo la Segerea zinahitaji mtu wa kujitoa ili kuwatumikia wananchi.
Aidha, amesema amevutiwa na wingi wa wasanii waliojitokeza kumpokea, ambapo amesema hivi karibuni atazindua "Rajab Amiry Foundation" huku akiwataka wasanii hao kila mmoja kuchangia walau 1000 ili waweze kutatua changamoto za Seregea na badae kufika katika mikoa yote nchini Tanzania .
0 Comments