Diwani wa CCM Kata ya Mzimuni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Manfred C. Lyoto amefariki dunia leo tarehe 7 Machi 2026
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, Abdalah M. Ally, ambaye pia ametoa pole kwa wanachama wa CCM pamoja na wananchi wote wa Kata ya Mzimuni na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kufuatia msiba huo.
Amesema taratibu za mazishi pamoja na taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.






0 Comments