NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ismani mkoani Iringa William Vangimembe Lukuvi leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya wananchi wa Jimbo la Ismani baada ya kuteuliwa na Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kuwa mgombea ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.
Lukuvi aliyeambatana na viongozi wa CCM wilaya ya Iringa vijijini wakiongozwa na katibu wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Sure Mwasanguti katibu wa itikati na uenezi wilaya hiyo Anord Mvamba na wengine walifika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ismani na KalengaCaroline Otieno majira ya saa 6:55 mchana leo jumapili.
Lukuvi akiwa mwenye furaha kubwa kutokana na kuaminiwa na chama Kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu Jimbo la Ismani alikabidhiwa mkoba maalum wenye fomu ya kugombea ubunge pamoja na miongozo ya tume huru ya uchaguzi.
Lukuvi amekuwa mteule wa kwanza Kuchukua fomu katika wilaya ya Iringa vijijini yenye majimbo mawili jimbo la Ismani na Kalenga ambalo mteule wake ni Jackson Kiswaga.
0 Comments